Psalms 106:35-40


35 abali walijichanganya na mataifa
na wakazikubali desturi zao.

36 bWaliabudu sanamu zao,
zikawa mtego kwao.

37 cWakawatoa wana wao
na binti zao dhabihu kwa mashetani.

38 dWalimwaga damu isiyo na hatia,
damu za wana wao na binti zao,
ambao waliwatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani,
nayo nchi ikanajisika kwa damu zao.

39 eWakajinajisi wenyewe kwa yale waliyotenda;
kwa matendo yao wenyewe wakajifanyia ukahaba.


40 fKwa hiyo Bwana akawakasirikia watu wake
na akauchukia sana urithi wake.
Copyright information for SwhKC